Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 09Article 584503

Soccer News of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Liverpool yaichapa 4-1 Shrewsbury Kombe la FA

Kinda wa Liverpool Kaide Gordon akishangilia goli la kuisawazishia Liver Kinda wa Liverpool Kaide Gordon akishangilia goli la kuisawazishia Liver

Liverpool imeibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya timu ya Ligi daraja la kwanza Shrewsbury katika mchezo wa hatua ya tatu ya Kombe la FA uliopigwa dimba la Anfield Leo Jumapili Januari 9.

Ushindi huo kwa Mabingwa mara saba wa Kombe la FA ulitanguliwa kutiwa doa kufuatia bao la mapema la Daniel Udoh kabla ya Liverpool baadaye kuamka na kurejesha bao na kuongeza nyingine tatu.

Mabao ya Majogoo wa Jiji la Merseyside Liverpool yamewekwa kimiani na kinda Kaide Gordon, Fabinho alifunga kwa njia ya penati, Roberto Firmino na ushindi mnono ukihitimishwa ba Fabinho tena na kufanya matokeo kuwa 4-1.