Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 26Article 559741

Soccer News of Sunday, 26 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Liverpool yakwaa kisiki, yalazimishwa sare ugenini

Wachezaji wa Brentford wakishangilia goli dhidi ya Liverpool. Wachezaji wa Brentford wakishangilia goli dhidi ya Liverpool.

Majogoo wa Jiji klabu ya Liverpool, wamekwaa kisiki katika mfululizo wa michezo ya ligi kuu England baada ya kulazimishwa sare ugenini katika uwanja wa Brentford Community dhidi ya Brentford.

Mchezo huo ambao uliisha kwa sare ya magoli 3-3, uliwaacha wengi wakiwa hawaamini kwani tangu kuanza kwa msimu wa 2021/2022, Liverpool wamecheza michezo mitano wakishinda michezo minne na kusuluhu mchezo mmoja dhidi ya Chelsea.

Brentford ambao wamepanda daraja msimu huu hawakuwa na uoga katika kulishambul;ia lango la Liverpool kwani muda mwibgi walikua wakipeleka hatari kwa walinzi wa Liver.

Magoli ya Liverpool katika mchezo huo yamefungwa na Diogo Jota, Mohamed Salah na Curtis Jones huku yale ya Brentford yakifungwa na Pinnock, Janelt na Wissa.

Liverpool ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 14 wakiwa wameshacheza mechi 6.