Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573169

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Liverpool yatibua rekodi ya Arsenal, yaichapa goli 4

Liverpool yaichapa Arsenal Liverpool yaichapa Arsenal

Majogoo wa Jiji, timu ya Liverpool wameibuka na ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumamosi Uwanja wa Anfield.

Mabao ya Wekundu wa Anfield, yamefungwa na Sadio Mane dakika ya 39, Diogo Jota dakika ya 52, Mohamed Salah dakika ya 73 na Takumi Minamino dakika ya 77.

Kabla ya mchezo wa jana Jumamosi, Arsenal wamecheza michezo 10 katika mashindano yote pasipo kupoteza.

Liverpool imefikisha pointi 25 baada ya ushindi huo na kurejea nafasi ya pili ilizidiwa pointi nne na vinara, Chelsea baada ya wote kucheza mechi 12, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 20 za mechi 12 pia nafasi ya tano.