Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 585031

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Luka Modric amejihakikishia nafasi Real Madrid?

Kiungo wa Real Madrid, Luka Modric Kiungo wa Real Madrid, Luka Modric

Luka Modric anaonekana kuwa tayari kusalia Real Madrid. Modric amekuwa n Real Madrid tangu 2012, akifanikiwa kushinda mataji mawili ya La Liga, manne ya Ligi ya Mabingwa na mengine mengi.

Kiungo huyo amekuwa nguzo kuu katika klabu ya Real Madrid kwa kipindi cha muongo mmoja, na hata akiwa na umri wa miaka 36, ​​haonyeshi dalili za kupungua ubora wake.

Msimuu huu Modric ameendelea kuonesha kiwango cha kimataifa, huku Real Madrid wakiwa kileleni mwa La Liga hadi sasa.

Kwa mujibu Diario AS, Real Madrid tayari wameamua kuongeza mkataba wa Modric hadi msimu wa joto wa 2023.

Ripoti hiyo inadai kuwepo kwa makubaliano tangu majira ya joto juu ya nyongeza ya mwaka mmoja kwa mshahara pungufu kwa 10% ya mkataba.

Iwapo kandarasi hiyo itasainiwa, Modric ataendelea kuwa na Real Madrid hadi atakapofikisha umri wa miaka 37, na huenda akastaafu soka akiwa Santiago Bernabeu.