Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 22Article 558910

Habari za michezo of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Lwandamina Arudisha Jeshi Lake Kambini

Lwandamina Arudisha Jeshi Lake Kambini Lwandamina Arudisha Jeshi Lake Kambini

KOCHA Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina, baada ya kufanikisha timu hiyo kuvuka hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, jana amerudisha kambini jeshi lake kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

Azam imefanikiwa kuiondosha Horseed ya Somalia kwa jumla ya mabao 4-1 katika mchezo wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo sasa inakwenda kucheza dhidi ya Pyramid ya Misri.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Timu kwa sasa haipo kambini ila tunatarajia kuanza rasmi kambi yetu kesho (leo) kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya ligi kuu kwa msimu ujao.

“Majeruhi waliopo kwenye kikosi ni wawili tu ambao ni Prince Dube ambaye alifanyiwa upasuaji hivi karibuni na Charles Zulu, ila wengine wote wapo vizuri.”