Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572527

Habari za michezo of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: eatv.tv

Lwanga mchezaji bora Uganda 2021

Lwanga mchezaji bora Uganda 2021 Lwanga mchezaji bora Uganda 2021

Kiungo wa Simba na timu ya taifa ya Uganda, Taddeo Lwanga amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Uganda wa mwaka 2021 wa tuzo zinazotolewa na jarida la michezo la Football 256 la nchini humo na kuwapiku Eric Kambale (Express FC) na Yunus Sentamu (Vipers FC).

Taddeo ameshinda baada ya kupigiwa kura 468, 631 kati ya kura 1,124, 568 zilizopigwa wakati Erick Kambale amekuwa wapili kwa kura 399, 426 huku Sentamu akiwa watatu kwa kupata kura 256, 529.

Lwanga anakuwa mchezaji watatu kubeba tuzo hiyo tokea kuanzishwa kwake baada ya Allan Okello (KCCA) kushinda 2019 na Nicholas Wadada (Azam FC) kushinda mwaka 2020.