Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 09Article 541720

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MAJALIWA KUFUNGUA UMITASHUMTA, UMISSETA

Leo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza-nia, Kassim Majaliwa anafungua Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA) kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Waziri Mkuu anafanya ufunguzi wa mashindano haya kwa mara ya kwanza kwenye historia ya Tanzania ambapo yame-boreshwa kwa kiwango cha juu kwa uratibu wa Wizara tatu tofauti na miaka yote tangu kuanzishwa kwake. Akiwasilisha hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bungeni hivi karibuni, Waziri mwenye dhamana hiyo, Innocent Bashungwa amesema Serikali imeratibu mashindano hayo kwa kuzishiriki-sha Wizara zinazohusika na Habari, Elimu na TAMISEMI ili kuboresha michezo nchini.

Tayari timu ya Makatibu Wakuu wa Wiz-ara hizo wametoa taarifa kwa umma kuhusu namna serikali ilivyojipanga katika kuhak-ikisha kwamba mashindano ya mwaka huu yanafanyika katika ubora wa kiwango cha juu tofauti na hapo awali.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema mashindano hayo yal-ianza Juni 6-19, 2021 na yatafungwa Julai 3, mwaka huu. “Jumla ya washiriki wapatao 3,600 kutoka mikoa yote Tanzania Bara wanatarajiwa kushiriki katika michezo ya UMITASHUMTA na washiriki 3,800 kutoka Mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar watashiriki katika michezo ya UMISSETA,” amefafanua Prof. Shemdoe.

Ameitaja michezo itakayohusika kuwa ni mpira wa miguu, neti-boli, mpira wa wavu, mpira wa mikono, mpira wa meza, riadha jumuishi, kwaya na ngoma. Kikapu itahu-sisha shule za Sekondari kwa wavulana na wasichana. Ameongeza kwamba umuhimu wa UMITASHUMTA na UMISSETA ni kuvumbua vipaji na kisha kuweka mikakati endelevu ya kuviendeleza ili kupata wachezaji wa timu za Taifa kwa michezo mbalimbali pia wataalamu wa michezo ambao watatokana na misingi imara ya taaluma ya michezo.

Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema miongoni mwa maboresho yaliyofanyika kwenye mashindano ya mwaka huu ni pamoja na kuyarusha mubashara kupitia vituo mbalimbali vya televisheni na mitandao ya kijamii hapa nchini. Amesema kwa sasa Serikali inatekeleza mradi wa kupanua na kuboresha Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ikiwa ni mkakati maalum wa kuanzisha kituo cha kimataifa cha kuendeleza vipaji vya mich-ezo nchini ambacho kinaweza kutumika kuivisha vipaji kutoka kwenye mashindano haya.

Dkt. Abbasi ameongeza kuwa Serikali im-eendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayowezesha Taasisi na watu binafsi wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika kuendeleza vituo vya kuvumbua na kuendeleza vipaji ambapo tayari Serikali imeanza mazungumzo na balozi mbalimbali kama za Brazil, Uturuki, Cuba na Misri ambazo zote zimeonyesha nia.

“Ni matumaini ya Serikali kuwa jitihada zote hizi zitazaa matunda ya kuwa na wachezaji wengi katika michezo mbalimbali na hivyo kuwa washindani wakubwa katika mashindano makubwa ya kimataifa kama Olimpiki, All Africa Games na Jumuiya ya Madola,” alisisitiza Dkt. Abbasi Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. James Mdoe, amesema Wizara hizi tatu kwa sasa zinafanya kazi kwa kushirikiana na tayari zimekuja na mkakati wa kutenga shule mbili katika kila mkoa ambazo zitafundisha somo la michezo katika ngazi ya kidato cha tano lakini pia zitatumika kama vitalu vya kukuza na kuendeleza vipaji vitakavyovumbuliwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati akili-hutubia Bunge Aprili 22, 2021 Jijini Dodoma alieleza kwamba Sekta ya Sanaa, Utamaduni na Michezo inakua kwa kasi kubwa na inatoa fursa ya ajira kwa vijana nchini hivyo Serikali yake imedhamiria kuboresha sekta hizo.Katika kuonyesha kuwa Serikali imejipanga kikamilifu Rais ameongeza kwamba Serikali yake itaanzisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, ili kuwa-sidia wasanii nchini kupata mafunzo na mikopo ambayo itasaidia kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Wakati akimwapisha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul, Rais Samia alisema alimteua kwenda katika Wizara hiyo ili akasimamie na kuendeleza michezo hususani timu za wanawake, jukumu alilokuwa akilifanya yeye wakati akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupewa na wajibu huo na Hayati Rais John Pombe Magufuli.Kwa hakika kazi inaendelea.

Mwandishi wa Makala haya ni John Mapelele, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo anapatikana kwenye [email protected] na 0784441180

Join our Newsletter