Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 12Article 585094

African Cup of Nations of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Maajabu 7 ya namba 9 Afcon

Maajabu 7 ya namba 9 AFCON Maajabu 7 ya namba 9 AFCON

Fainali za Afcon mwaka huu zinaendelea huko Cameroon ambapo leo ni siku ya tatu tangu zilipoanza rasmi, Januari 9 na zitafikia tamati, Februari 6.

Kuanza kwa fainali hizo tarehe 9 mwezi huu, kunaweza kuonekana ni jambo la kawaida lakini namba hiyo tisa ina maana kubwa katika fainali hizo.

Inawezekana wengi hawafahamu uzito na maana kubwa iliyobebwa na namba 9 katika fainali za Afcon na ifuatayo ni orodha ya mambo saba yanayoendana na namba tisa kwenye fainali za Afcon.

1. Wachezaji watatu wanaoongoza kwa kufunga idadi kubwa ya mabao katika fainali hizo, Samuel Eto'o wa Cameroon mwenye mabao 18, Laurent Pokou (Ivoy Coast) aliyefunga mabao 14 na Rashid Yekini (Nigeria) aliyefumania nyavu mara 13, kila mmoja alikuwa akivaa jezi namba 9 katika fainali hizi akiwa na timu yake ya taifa.

2. Idadi kubwa ya mabao kufungwa katika awamu moja ya fainali za Afcon ni tisa (9) ambayo yalipachikwa na Ndaye Mulamba wa DR Congo (zamani Zaire) katika fainali za 1974 zilizofanyika Misri.

3. Kocha aliyeshiriki fainali nyingi za Afcon ni Claude Le Roy raia wa Ufaransa ambaye amefanya hivyo katika fainali tisa (9) tofauti akiwa na timu za Cameroon, Senegal, Ghana, DR Congo, Congo na Togo.

4. Timu kutoka Kanda ya Afrika Magharibi (WAFU) kwa pamoja zimechukua kombe la Afcon mara tisa (9). Idadi hiyo ni sawa na jumla ya mataji ya Afcon yaliyochukuliwa na timu mbili tu kutoka Kanda ya Kaskazini (UNAF), Misri na Algeria ambazo kwa pamoja zimebeba ubingwa mara tisa.

5.Wenyeji Cameroon ni miongoni mwa timu zilizonusa mara nyingi hatua ya nusu fainali ya Afcon wakifanya hivyo mara tisa (9).

6.Misri na Ghana ndio timu zilizofika mara nyingi katika hatua ya fainali ya mashindano ya Afcon ambapo kila moja imefika fainali mara tisa (9)

7. Ni wachezaji watatu tu katika fainali zinaoendelea za Afcon wanaovaa jezi namba tisa (9) huku wakiwa sio washambuliaji ambao ni viungo Abdel Raouf wa Sudan na Youssouf M'Changama pamoja na beki wa Burkina Faso, Issa Kabore.