Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 21Article 558772

Soccer News of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Maandalizi mchezo wa ngao ya hisani yamekamilika 100% - Almas Kasongo

Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo

Wakati dirisha la Ligi Kuu likienda kufunguliwa Septemba 27, kuna mchezo unaoashiria ufunguzi wa Ligi kuu na safari hii mchezo huo utakuwa ni baina ya mahasimu wawili wa soka la Tanzania, Simba Sc na Yanga Septemba 25.

Mchezo wa "Derby" safari hii utapigwa kwa mkapa Jijini Dar es Salaam, uwanja ambao mashabiki wa vilabu hivi huomba ufanyikie hapo mchezo huo.Mchezo huo ni wa Ngao ya hisani.

Sasa katika kuelekea mchezo huo Bodi ya Ligi kupitia kwa mtendaji wake Mkuu Almasi Kasongo wamesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa 100%.

"kama unavyofahamu mwaka huu tumekuwa na maandalizi kuanzia kwa waamuzi, na watu wote wanaohusika kwenye mchezo wa mpira wa miguu huku lengo likiwa ni kuweka mazingira sawa ya mchezo huu"

"Katika changamoto ya suala la tiketi tumeendelea kushughulikia na ndio maana unaona katika matukio mawili yaliyopita (Yanga Day na Simba Day) suala la tiketi hukusikia kelele.

"Na bado tunajaribu kufanya vikao na kila anaehusika katika mchezo huo ili tuweze kujua ana changamoti ipi,lengo letu ni ikifika siku ya mchezo basi kila changamoto itakayoibuka iwe ni changamoto mpya" amesisitiza Kasongo