Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 13Article 551335

Soccer News of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Maandalizi ya Ubingwa Yanga 100%

Nyota Mpya wa Yanga, Bryson David Nyota Mpya wa Yanga, Bryson David

Ni wazi sasa Yanga wanaonesha kwa vitendo wamepania kwa dhati kuupoka ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara 2020/2021 kutoka kwa wapinzani wao Simba SC walioubeba mara nne mfululizo.

Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kumtambulisha nyota wao mpya David Bryson ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya KMC, huku huo ukiwa ni muendelezo katika kukisuka kikosi chao cha Mapambano kwa msimu Mpya unaokuja wa Ligi.

Beki huyo wa kushoto ni moja ya wachezaji waliokuwa tegemeo ndani ya KMC anaungana na mzawa mwingine Dickson Ambundo ambaye alitambulishwa mapema siku ya Jumatano wiki hii.

Bryson amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia Wananchi ambao wapo chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa bado usajili unaendelea na kwa sasa ni nyota wawili wa kimataifa wamebaki kutambulishwa rasmi.

Ndani ya wiki hii pekee Yanga imetambulisha nyota Djigui Diarra,Khalid Aucho,Dickson Ambundo na Erick Johola kama sehemu ya kikosi cho Msimu ujao.

Wakati hayo yanaendelea, Alfajiri ya leo Agosti 13 Djuma Shaban na Jesus Moloko tayari wamewasili Dar es Salaam kukamilisha taratibu za kujiunga na Klabu ya Yanga.