Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 09Article 584446

Soccer News of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Madrid yaitandika 4-1 Valencia La Liga

Wachezaji wa Real Madrid wakipongezana Wachezaji wa Real Madrid wakipongezana

Real Madrid imeongoza utawala wa alama kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga kufuatia kutoa kichapo cha goli 4-1 dhidi ya Valencia wakiwa nyumbani na sasa tofauti ya alama nane na timu iliyonafasi ya pili.

Kikosi cha kocha Carlo Ancelotti kilipata uongozi na kutawala mchezo huo kupitia bao la mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Karim Benzema kwa njia ya penati baada ya kiungo mkabaji wa Brazil Casemiro kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari muda mfupi kabla ya mapumziko.

Madrid wakarudi wakiwa bora teba ungwe ya pili ambapo winga wa Vinicius Junior kufunga goli mbili na sasa Valencia wakapata bao la kufutia machozi kupitia kwa Goncalo Guedes ambaye alifunga kwa kichwa akimalizia ‘rebound’ baada ya penati kuokolewa.

Hata hivyo, bao la 301 la Karim Benzema liliondoa dhana ya uwezekano wa kurudisha goli kwa Valencia.

Ushindi huo unaifanya Real Madrid kuketi kileleni mwa msimamo wa La Liga kwa tofauti ya alama nane kwa Sevilla ambao wanamichezo miwili mkononi, Sevilla watakuwa na mchezo Jumapili dhidi ya Getafe.