Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573214

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Madrid yajipanga kwa Mbappe na Rudiger

Rudiger mpaka sasa hajasaini mkataba mpya na Chelsea Rudiger mpaka sasa hajasaini mkataba mpya na Chelsea

Imekuwa bayana kwa takribani miaka miwili sasa nyota wa PSG, Kylian Mbappe anataka kuhamia klabu ya Real Madrid, na klabu hiyo tayari imeonesha nia ya kuipata saini yake.

Mbappe hajakubali kusaini mkataba mpya na klabu yake kwa sasa, na iko wazi kuwa Real Madrid wanatarajia kumpata akiwa kama mchezaji huru baada ya kukamilisha mda wake klabuni hapo.

PSG bado hawajakubali kukata tamaa na kuachana na staa huyu. Inatarajiwa kutakuwa na mvutano kidogo mpaka upande mmoja utakapokuwa na uhakika wa kuwa naye kwa muda zaidi kwa mkataba mpya.

Hata hivyo, imeripotiwa kuwa vita yao nyingine inaenda kuwa juu ya saini ya Antonio Rudiger, ambaye kwa sasa anamilikiwa na klabu ya Chelsea, na amevivutia vilabu vyote viwili.

Rudiger mpaka sasa hajaamua kukubali mkataba uliowekwa mezani na Chelsea, na bila shaka anataka kujua ofa zitakazo wasilishwa na vilabu vikubwa Ulaya, ili aweze kuchagua ofa bora kwake.