Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 09Article 541909

Habari za michezo of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Majaliwa atetea 'mapro' kukipiga Ligi Kuu nchini

Majaliwa atetea 'mapro' kukipiga Ligi Kuu nchini Majaliwa atetea 'mapro' kukipiga Ligi Kuu nchini

- wanapaswa kujielekeza kwanza katika kukuza vipaji kuanzia ngazi ya msingi.

Aidha, amesema nyota wa kigeni wanaongeza ushindani kwa wachezaji wa ndani hali inayofanya michezo iwe na msisimko tofauti na kuwaacha wazawa peke yao.

Majaliwa alitoa kauli hiyo jana mkoani Mtwara, wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania (Umitashumta na Umisseta), ambayo kitaifa yanafanyika mkoani hapa, yakiwa na kaulimbiu ya "Michezo Sanaa na Taaluma kwa Maendeleo ya Viwanda na Uchumi".

“Tukiwaacha wachezaji kutoka nje, hatutakuwa na ushindani sahihi hususan katika soka kwa sasa, hivyo tuimarishe kwanza wachezaji wetu wa ndani kabla ya kufikiria kuachana na wa nje,” alisema Majaliwa.

Aliongeza kuwa jamii haikuwaanda watoto ipasavyo kuwa wanamichezo imara wa siku zijazo, na kwamba ni wakati wa kubadilika ili matokeo ya michezo hiyo ya Umitashumta na Umisseta  yaonekane.

“Serikali italivalia njuga jambo hili kuanzia ngazi ya chini kwa ajili ya kupata matokeo bora kwenye michezo na sanaa,”alisema Majaliwa

Aliwataka washiriki wa michezo hiyo ya kutambua kuwa michezo ni ajira na wahakikishe wanatumia fursa hiyo kuonyesha vipaji vyao kwa ajili ya kuvutia wafuatiliaji wa vipaji vya michezo mbalimbali.

Azipa wizara tatu angalizo

Pia Majaliwa amezipa angalizo Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Tamisemi, kuhakikisha ari na msisimko ulioonyeshwa wakati wa ufunguzi wa michezo hiyo mkoani Mtwara haupotei kila mashindano hayo yanapofanyika.

Alisema wizara hizo zinapaswa kuhakikisha ushiriki wa michezo hiyo inakuwa endelevu wakati wote kwa kuwa inaipunguzia serikali gharama za kuwatibu watu wake kutokana na kutokufanya mazoezi

 

Awaasa Wanafunzi

Aidha Majaliwa, aliwaasa wanafunzi wanaoshiriki michezo hiyo ya Umitashumta na Umisseta, watambue kuwa mpaka kufikia hatua hiyo wamepitia michakato mbalimbali kwa ajili ya vipaji walivyonavyo, hivyo wahakikishe hawabweteki.

Aliwaonya kutojiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa jambo hilo ni kosa kisheria, lakini pia huua vipaji vingi vya wanamichezo wanaochipukia

Alisema ni wakati wa kuwapata kina Mbwana Samatta, Kelvin John, Diamond Platnumz, Ali Kiba, Harmonize na kina Peter  Msechu wengine watakaowakilisha Tanzania kimataifa katika nyanja mbalimbali za michezo na sanaa kimataifa.

Join our Newsletter