Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 22Article 547825

Habari za michezo of Thursday, 22 July 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Makambo, Mayele Waaga Ishu Ya Kutua Yanga

Makambo, Mayele Waaga Ishu Ya Kutua Yanga Makambo, Mayele Waaga Ishu Ya Kutua Yanga

Makambo, Mayele Waaga Ishu Ya Kutua Yanga July 21, 2021 by Global PublishersRASMI sasa hivi mshambuliaji wa AS Vita, Fiston Mayele na Heritier Makambo anayekipiga Horoya AC wanatua Yanga ni baada ya nyota hao kuwaaga mashabiki wa klabu zao.


Awali zilikuwa tetesi pekee, lakini hivi sasa rasmi nyota wanakuja Yanga baada ya kufikia muafaka mzuri wa kuja kukipiga Jangwani katika msimu ujao.

Yanga wanawasajili washambuliaji hao kwa ajili ya kuiimarisha safu yao ya ushambuliaji watakaokuja kuchukua nafasi za Fiston Abdulrazack na Michael Sarpong.

Kwa kupitia ukurasa wa kijamii wa Horoya, uliweka picha na ujumbe na picha ya kumuaga Makambo uliosomeka hivi: “Misimu miwili baada ya kuwasili kwako, sisi kama klabu tumemaliza ushirikiano.“Tunakushukuru kwa utumishi wako mwaminifu, weledi wako na tunakutakia kila la kheri katika kazi yako yote. Asante.”

Hiyo ni ishara tosha kuwa mshambuliaji huyo anakuja kuki–piga Yanga, hivi karibuni gazeti hili liliandika taaraifa za Makambo kuandika barua ya kusitisha mkataba wake wa mwaka mmoja alioubakisha kwa ajili ya kwenda kutafuta changamoto nyingine kwingine na ndiyo kilichotokea nyota huyo mkataba wake umevunjwa baada ya maku–baliano ya pande mbili mchezaji na klabu.

Hiyo imejitokeza kwa Mayele ambaye yeye aliwaaga vion–gozi na mashabiki wa AS Vita kwa kupitia ukurasa wake wa mtandao ya kijamii kwa kusema kuwa: “Niwashukuru mashabiki wa AS Vita kwa kuwepo hapa kwa kipindi chote, nakwenda kutafuta changa–moto nyingine kwingine.

”Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinaeleza kuwa, Mayele na Makambo muda wowote watatua nchini kwa ajili ya kuwahi maandalizi ya msimu mpya ambao watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika inayotarajiwa kuanza mwezi Septemba

Share this:TweetWhatsApp Related