Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 23Article 553015

Habari za michezo of Monday, 23 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Makamu wa Rais riadha ajiuzulu

Makamu wa Rais riadha ajiuzulu Makamu wa Rais riadha ajiuzulu

John Bayo amejiudhuru nafasi ya makamu wa rais kwenye Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Katibu mkuu wa RT, Jackson Ndaweka ameithibitishia Mwananchi Digital kujiuzulu kwa Bayo.

Amesema ni baada ya kushaurina na familia yake na kuchukua hatua hiyo kwa kile alichodai ni kutingwa na majukumu mengine.

Awali baadhi ya wadau wa riadha waliwahi kumlalamikia Bayo BMT kuwa hana sifa ya elimu kama katiba ya RT inavyotaka, madai ambayo aliyakanusha.

"Amejiuzulu na tayari ametoa taarifa, nafasi yake itatangazwa na itagombewa kwenye uchaguzi mdogo wakati wa mkutano mkuu wa kawaida wakati wowote kuanzia sasa," amesema Ndaweka.