Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 586048

African Cup of Nations of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Malawi Yatoa Kipigo kwa Zimbabwe Afcon 2021

Malawi waliibuka na ushindi dhidi ya Zimbabwe Malawi waliibuka na ushindi dhidi ya Zimbabwe

Timu ya taifa ya Malawi imeichapa bao 2-1 timu ya taifa ya Zimbabwe ambapo mshambuliaji Gabadinho Mhango amefunga goli mbili na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa kwanza Kundi B na kutengeneza matumaini ya kufuzu kwa mara ya kwanza hatua ya 16 bora.

Zimbabwe walitangulia kupata goli kupitia kwa Ishmael Wadi kunako dakika ya 38 kabla ya Mhango kusawazisha goli hilo ikiwa ni baada ya dakika tano pekee.

Mhango aliipa uongozi the Flames ikiwa ni dakika 13 tangia kuanza kipindi cha pili.

Kundi B kwa sasa limekaa mseto ambapo Malawi anakuwa na alama tatu wakati kileleni kuna Guinea na Senegal ambazo zote zina alama nne baada ya ushindi wa mechi moja na sare.

Mechi ya mwisho Malawi watakuwa uwanjani na Senegal Jumanne sawa ba Zimbabwe dhidi ya Guinea.