Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 22Article 573307

Soccer News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Man City ni mwendo wa kimya kimya EPL

Mfungaji wa moja ya Magoli ya City Mfungaji wa moja ya Magoli ya City

Mabingwa watetezi wa EPL, Manchester City wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad.

Mabao ya Man City katika kipute hicho yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya 44, Rodri dakika ya 55 na Bernardo Silva dakika ya 86.

Kwa ushindi huo, Man City wanafikisha pointi 26, wakizidiwa tatu na vinara, Chelsea baada ya wote kucheza mechi 12.