Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572869

Soccer News of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Man City yamgeukia De Jong

Franke de Jong Franke de Jong

Manchester City wameripotiwa kuwa wamewasilisha ofa rasmi ya Euro milioni 90 (Pauni milioni 75) kwa nyota wa Barcelona Franke de Jong.

De Jong amekuwa mchezaji muhimu wa Barcelona tangia alipowasili klabuni hapo mwaka 2019.

Hata hivyo, licha ya umuhimu wa Frenkie de Jong Barca, kumekuwa na mawazo kuwa anaweza kuweka sokoni ili kupunguza changamoto ya kifedha klabuni hapo.

Uwepo wa Gavi na jitihada zake zinahatarisha hatma ya nafasi ya De Jong kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona ikiwa Pedri atarejea kutoka kuuguza majeraha.

Nyota huyu mwenye uraia wa Uholanzi, atakuwa kama mchezaji wa ziada, na bila shaka anahitaji muda zaidi wa kucheza kwa upande wake.

Kwa mujibu wa chapisho la Fichajes, ambao walikuwa wakivutiwa na staa huyu kwa muda sasa tangia alipokuwa Ajax, wamejaribu kuwasilisha ofa yao kwa Barcelona ya Euro milioni 90.

Taarifa inataja kuwa bila shaka Barcelona watakuwa tayari kumuachia Frenkie de Jong aondoke, na kutengeneza faida ya Pauni milioni 10.