Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 559969

Soccer News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Man United haichezi kitimu, ngumu kushinda taji, waendelee na Ole - Neville

Gary Neville Gary Neville

Gwiji wa zamani wa Manchester United na Mchambuzi wa Soka wa Kituo cha Sky Sports, Gary Neville amesema ni ngumu kwa kikosi cha United kushinda mechi zao kwa kuwa hawachezi kitimu lakini cha msingi waendelee kumpa nafasi kocha Ole Gunner Solkjaer.

United imepoteza mechi yake ya tatu katika mechi nne zilizopita za mashindano yote baada ya kupoteza mechi dhidi ya Aston Villa nyumbani siku ya Jumamosi, kabla walitolewa katika michuano ya Carabao Cup raundi ya tatu baada ya kupoteza mbele ya West Ham.

Akizungumza hivi karibuni, Gary Neville amesema Man United lazima ihakikishe inacheza kitimu, kwa umoja kama wanahitaji kupambana kwa ajili ya kushinda mataji na lazima wapate taji ndani ya miezi 18 ijayo.

Baada ya usajili wa Cristiano Ronaldo, Jadon Sancho na Raphael Varane majira ya kiangazi kuna shinikizo kwa klabu kushinda mataji. Neville anaamini timu itaona matunda ya Ole Gunners kwa kuwa kitendo cha kufukuza walimumara kwa mara hakikuweza kusaidia.

Nimekuwa nikisema hiki wanaposhinda,nimesema wakati Ronaldo anapofunga magoli hawachezi kama timu inayoweza kushinda ubingwa kwa maono yangu.

Mnahitajika kuwa na muungano mnapokuwa na mpira na baada ya kupoteza mpira, mnahitaji mtiririko wa uchezaji na mnahitaji kuwa na mtindo wa uchezaji.

Neville amewahi kucheza na Kocha wa sasa wa Man United wakiwa Chini ya Kocha. Sir Alex Ferguson.