Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 26Article 559708

Soccer News of Sunday, 26 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Man United hoi EPL, Kocha anyooshewa kidole

Aston Villa wakishangilia goli lao dhidi ya Man United Aston Villa wakishangilia goli lao dhidi ya Man United

Mashetani wekundu, Man United wameshuhudia jahazi lao likizama mbele ya Aston Villa baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0.

Man United wamepoteza mechi yao ya Pili mfululizo baada ya kati kati ya wiki kushuhudia wakitolewa katika kombe la Carabao dhidi ya West Ham katika dimba hilo hilo la Old Trafford.

Goli la Aston Villa katika mchezo huo liliwekwa wavuni na K. Hause dakika za mwisho za mchezo huku kiungo Mreno wa timu hiyo, Bruno Fernandes akikosa mkwaju wa penati.

Lawama nyingi juu ya matokeo mabovu ya timu hiyo anasukumiwa mwalimu Ole Gunner Solkjaer, hasa baada ya kikosi hicho kufanya usajili mzuri msimu uliopita lakini bado matokeo yake ni ya kusuasua uwanjani.

Wengi wanalalamikia mbinu mbovu za Solkjaer huku wakipigia chapuo kikosi hicho kimuajiri Antonio Conte ama Zinedine Zidane ambao wote hawana kazi kwa sasa baada ya kuachana na vikosi vyao msimu uliopita.