Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573091

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Man United wajadili kipengele cha kuvunja mkataba wa Ole Gunnar

Meneja wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer Meneja wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer

Klabu ya machester United imeamua kuachana na Kocha wake Ole Gunnar Solskjaer kama Kocha wa kikosi hicho baada ya kipigo cha magoli 4-1 ugenini dhidi ya Watford.

Mkutano wa dharura wa bodi ya wakurugenzi umeitishwa na wamiliki wa timu hiyo, familia ya Glazer baada ya kipindi cha kwanza wakati wa mchezo dhidi ya Watford na miongoni mwa mazungumzo yaliyozungumzwa katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Bodi Richard Arnold aliagizwa kufanya makubaliano ya vipengele vya kuvunja mkataba na raia huyo wa Norway.

Mkataba wa Ole utaigharimu Man United kiasi cha Pauni milioni 7.5 kama fidia ya kuvunja mkataba.

Solskjaer alisaini Mkataba wa mpya wa miaka mitatu August mwaka huu, na iwapo atatimuliwa basi mkongwe mwingine wa klabu hiyo Darrwn Fletcher atashika majukumu hayo kwa muda.