Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 584806

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Man United yafuzu raundi ya nne Kombe la FA

Kiungo wa Man United Scot McTominay Kiungo wa Man United Scot McTominay

Manchester United wamefanikiwa kutimba duru ya nne ya Kombe la FA England kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Aston Villa katika mchezo uliopigwa dimba la Old Trafford usiku wa Jumatatu, Januari 10.

Bao pekee kwenye mechi hiyo limefungwa na kiungo mkabaji Scot McTominay kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na kiungo mkabaji raia wa Brazil Frederico Rodrigues de Paula Santos ‘Fred’.

Kwa ushindi huo, The Red Devils watacheza dhidi ya Middlesbrough. Klabu ya Man United inaungana na Manchester City, Liverpool, West Ham United na timu nyingine.