Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 24Article 553498

Habari za michezo of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Manara: Naweka nguvu zangu Yanga

Manara: Naweka nguvu zangu Yanga Manara: Naweka nguvu zangu Yanga

BAADA ya kutambulishwa na uongozi wa Yanga, aliyekuwa ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema nguvu alizokuwa anazitumia Simba amezihamishia kwa mabosi wake wapya.

Manara amesema alikuwa anatumia nguvu nyingi Simba lakini wakawa wanamchukulia kawaida na nguvu hizo zitaanza kuonekana.

“Wapo wanasema ni klabu kubwa, hayo yote hayawezi kuwezekana kama hakuna watu hivyo vyote haviwezekani,” anasema Manara.

Manara amesema kuwa Yanga ni kama hisani kwa sababu viongozi wote wa klabu hiyo wanajua nilikuwa Simba.

“Nimevaa jezi ya Yanga na nimeambatana na familia yangu yote nawashukuru sana kwa kuniunga mkono hata huku nilipokuja, nimevaa jezi ya Yanga na sasa nipo huku,” anasema Manara.