Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 23Article 573742

Soccer News of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Manara afunguka udhamini wa GSM Ligi Kuu, agusia suala la "Fair Competition"

Balozi wa bidhaa za GSM, Haji Manara play videoBalozi wa bidhaa za GSM, Haji Manara

Msemaji kunako Klabu ya Yanga na "Brand Ambasador" wa bidhaa za Kampuni za GSM, Haji Sunday Manara "Bugati" ni miongoni mwa wadau waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu kati ya TFF na Kampuni ya GSM.

Haji ameelezea kwa undani furaha yake katika suala kama hilo kwa kuwa anaona nia ya dhati ndani yake iliyolenga kusaidia vilabu shariki vya Ligi Kuu.

Vile vile Haji alipata wasaa wa kuelezea kiundani suala la dhana ya "Fair Competition" ambayo imekua ikipigiwa kelele hasa baada ya Kampuni hiyo hiyo ya GSM kudhamini ama kufanya kazi na kampuni zaidi ya moja zinazoshiriki Ligi Kuu.

Tazama video na alichokisema zaidi Haji Manara.