Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 24Article 553465

Soccer News of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Manara rasmi atambulishwa Yanga

Haji Manara, akiwa katika jezi ya Yanga Haji Manara, akiwa katika jezi ya Yanga

Aliyekuwa Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara leo Agosti 24, 2021 amejiunga na klabu ya Yanga huku akitoa ahadi kushirikiana na yanga katimu msimu mpya wa 2021/22 kuhakikisha Yanga inafikia malengo iliyojiwekea.

“Baada ya kutanga kuondoka Simba nilipokea ofa kutoka klabu nyingi, Yanga walivyonitafuta nilishangaa sana, nikawauliza malengo yao ni yapi, nimejiunga na klabu yenye mipango ya kushinda makombe,”amesema haji

"Nafurahi kujiunga na Klabu kubwa kuliko Klabu yoyote afrika mashariki, lakini Nafurahi kujiunga na timu ambayo itakwenda kushinda mataji yote msimu ujao,"

Haji alijiuzuru nyadhifa zake ndani ya simba mwezi uliopita baada ya kutoelewana na viongozi wa Simba SC.