Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 13Article 557200

Soccer News of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Manara uso kwa uso na viongozi wa Simba Karimjee

C.E.O wa Simba, Babra Gonzales na Msemaji wa Yanga Haji Manara wakisaini Kitabu cha Maombolezo C.E.O wa Simba, Babra Gonzales na Msemaji wa Yanga Haji Manara wakisaini Kitabu cha Maombolezo

Aliekuwa Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amekutana uso kwa uso na viongozi wa Simba Sports Club katika kuaga mwili wa aliekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Zacharia Hans Poppe aliefariki dunia Septemba 10 katika hopitali ya Agha Khan alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika Viwanja hivyo vya Karimjee amefika Mtendaji Mkuu wa Simba, Babra Gonzalez, MweNyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu na Viongozi wengine wa Simba.

Haji kwa Sasa ni Msemaji wa Yanga, Mahasimu wa Simba na katika moja ya Mazungumzo yake na vyombo vya Habari, mara kadhaa Haji amesikika akimzungumzia Babra kuwa ndio chanzo hasa cha yeye kuondoka ndani ya Klabu hiyo kutokana na kutokuwa na maelewano nae.

Haji Manara na Marehemu Zacharia Hans Poppe, wamefanya kazi katika klabu ya Simba kwa miaka yote sita ambayo Haji amehudumu kama Afisa Habari huku kwa kiasi kikubwa Hans Poppe akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili.