Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 25Article 574081

Soccer News of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Manchester United kumteua Ralf Rangnick kuwa kocha wa muda

Ralf Rangnick Ralf Rangnick

Klabu ya Manchester United ambayo kwa sasa haina Kocha baada ya kumtimua Ole Gunnar Solskajaer wiki iliyopita, imeanzisha mazungumzo na Mjerumani Ralf Rangnick kuja kuziba nafasi ya Ole Gunnar mpaka mwisho wa msimu.

Rangnick amewahi kuvifundisha vilabu vya Hoffenheim, RB Leipzig vinavyoshiriki Ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundasliga.

Rangnick kwa sasa anafanya kazi kama mkurugenzi wa maendeleo ya soka katika klabu ya Lokomotiv Moscow ya nchini Urusi.