Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 584794

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mane apeleka Kilio Zimbabwe, waichapa goli la dakika za jioni

Sadio Mane akiifungia Senegal bao la ushindi Sadio Mane akiifungia Senegal bao la ushindi

Bao pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Sadio Mane kwa njia ya penati limeipa ushindi finyu timu hiyo mbele ya Zimbabwe katika mchezo wa hatua ya makundi mtanange wa kwanza.

Ushindi kwa Senegal ni maumivu makubwa kwa Zimbabwe ambao walikuwa kwenye ubora lakini pia tuta hilo limetokea wakati mchezo huo ukidhaniwa kuwa utamalizika kwa sare tasa.

Tuta hilo limeamuriwa wakati dakika nne zikiwa zimesalia kandanda kumalizika, ambapo mlinzi, Kelvin Madzongwe alishika mpira wakati akijaribu kuokoa shuti la Pape Gueye, kisha Mane anayekipiga kunako Liverpool kuipa ushindi Senegal ambao ni moja ya timu zinazopewa kipaumbele cha kutwaa ubingwa.