Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 13Article 551341

Soccer News of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Maneno ya Haji Manara baada ya Chama Kuondoka Simba SC

Aliekuwa Msemaji wa Simba Haji Manara (Kushoto) na Chama Aliekuwa Msemaji wa Simba Haji Manara (Kushoto) na Chama

Aliekuwa Afisa habari na Msemaji wa Mabingwa wa nchi Haji Manara, ametoa neno kutokana na kile kinachoonekana baada ya nyota wa Klabu ya Simba Clatous Chama kusajiliwa na Klabu ya Rs Berkane ya Morocco.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Manara ameandika;

"Niliiona miguu yako siku ya kwanza nikapagawa na ufundi wako.. Nakumbuka tukiwa Kitwe Zambia, Picha hiyo ya mbele ikatawala Katika mitandao na Magazeti ya kwenu.

Nakumbuka pia wakati tunarudi ukaniambia tutafuzu kwenye mechi ya marudiano, ahhhhh Mwamba ukafunga goli maridadi mno dhidi ya Nkana.

Real friend na Jirani yangu nikutakie kheri nyingi katika maisha mapya Morocco na naamini utafanikiwa

Nani aliniamini nilipokuita Mwamba wa Lusaka August 2018?

Hakika Tanzania ilishuhudia talent murua kwa miaka mitatu na itoshe kusema nitakumiss sana my heroe "