Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 29Article 560275

Boxing News of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Manny Pacquiao astaafu rasmi mchezo wa ndondi

Bondia anaeachana na mchezo huo, Manny Pacquiao Bondia anaeachana na mchezo huo, Manny Pacquiao

Bondia kutoka nchini Ufilipino, Manny Pacquiao ametangaza rasmi kustaafu mchezo huo ili kujikita zaidi katika ulingo wa Siasa.

Bondia huyo anayeshikilia mataji ya uzani tofauti katika mchezo wa Masumbwi ni Seneta nchini humo na tayari ametangaza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2022.

Katika pambano lake la mwisho, Pacquiao mwenye umri wa miaka 42, alipoteza dhidi ya bondia wa Cuba Yordenis Ugas mjini Las Vegas mwezi uliopita.

"Nilisikia kengele ya mwisho tu. Mchezo ulikua umeisha," amesema Pacquiao.

Katika video iliyowekwa katika mitandao ya kijamii, Pacquiao ameelezea kustaafu kwake kama "uamuzi mgumu" katika Maisha yake, akiongeza kuwa mchezo wa Masumbwi ulimpatia "nafasi ya kupigana na umaskini" na "ujasiri wa kubadilisha maisha zaidi".

Pia amewashukuru mashabiki wake, marafiki na wale wote waliomuunga mkono katika mchezo huo,hususan Mkufunzi wake wa muda mrefu Freddie Roach, ambaye alimtaja kama "familia yangu, kaka na rafiki".

"Sitasahau kile nilichofanya na kufanikisha maishani mwangu," amesema.

Pacquiao anatambulika kama bondia bora wa kulipwa duniani, akishinda mataji 12 katika mikanda minane tofauti na ni bondia wa pekee kushikilia ubingwa wa dunia kwa miongo minne.