Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 28Article 560224

Soccer News of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mashabiki Simba, Biashara wapigana chupa Karume

Mashabiki Simba, Biashara wapigana chupa Karume Mashabiki Simba, Biashara wapigana chupa Karume

KATIKA hali isiyotarajiwa ndani ya Uwanja wa Karume, Musoma, mashabiki wa Biashara United na Simba wamejikuta wakipondana chupa za maji wakati mchezo baina ya timu hizo mbili ukiendelea.

Hali hiyo ilitokea katika jukwaa moja lilopo katika Uwanja wa Karume  dakika za nyongeza ya mchezo huo baada ya nyota wa Simba Pape Sakho kuangushwa kwenye boksi la 18 la Biashara na beki Salum Kipaga na mwamuzi kuamua ipigwe Penalti.

Maamuzi hayo yaliwafanya mashabiki wa Simba jukwaani pale wainuke na kuanza kushangilia jambo ambalo ni kama liliwakera wale wa Biashara na kuanza kurushiana chupa.

Chupa zile zilirushwa kwa pande zote mbili na kuwafanya mashabiki wengi kushuka jukwaani pale na kukimbia na kwenda sehemu salama na kuendelea kuangalia mpira hadi dakika 90 zilipomalizika.

Hata hivyo John Bocco wa Simba ndiye alipiga penalti ile na kuokolewa na kipa wa Biashara James Ssetuba na sekunde chache baadae mpira ulimalizika kwa suluhu      na kurejesha amani.

Baada ya kumalizika kwa mechi ilie, mashabiki wa pande zote mbili walionekana kuzungumza na kutaniana kama hakijatokea kitu.