Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572737

Habari za michezo of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mashabiki Simba wambebea Masau Bwire maua

Mashabiki Simba wambebea Masau Bwire maua Mashabiki Simba wambebea Masau Bwire maua

Mashabiki wawili wa Simba kutoka Nyasaka wilayani Ilemela Mkoa wa Mwanza wamefika uwanja wa CCM Kirumba kuushuhudia mchezo wa timu yao dhidi ya Ruvu Shooting wakiwa wamebeba maua.

Wamesema maua hayo ni kwa ajili ya kumkabidhi Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire kwa kile walichoeleza kuwa ni kumpa pole kwa kipigo kizito atakachopokea leo jioni cha mabao 3-0.

Wamesema kutokana na kauli zake za kuichukulia poa timu yao ya Simba wameamua kuja na maua hayo ili yamfariji kwa atakachokutana nacho baadae.

Mashabiki wanaendelea kumiminika uwanjani uwanjani hapo ili kuzishuhudia timu hizo zikimenyana baadae saa 10 jioni.