Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 23Article 573751

Habari za michezo of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mashabiki Wataka Pitso Asajiliwe Kuinoa Man United

Pitso Pitso

Mashabiki wa mpira wa miguu nchini Afrika Kusini wameanzisha kampeni mitandaoni wakishinikiza Kocha bora wa Nchi hiyo Pitso Mosimane kupewa kazi ya kuwa Kocha katika klabu ya Manchester United .

Baada ya matokeo mabaya mfululizo Manchester ilimfuta kazi Ole Gunnar Solskjaer huku Makocha kadhaa wakihusishwa kuchukua mikoba yake lakini Afrika Kusini wanaamini Kocha wao Mosimame anaweza kuivusha Klabu hiyo.

Picha zinazomuonesha Mosimane akiwa amevaa nguo zenye nembo ya Manchester United zimeendelea kusambazwa, Kocha huyo kwa sasa anaifundisha Al Ahly ya Misri na rekodi yake inatajwa kuwa bora.

Unadhani Pitso anafaa kuwa Kocha mkuu wa Manchester United?