Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 29Article 554236

Soccer News of Sunday, 29 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mastaa Yanga wapewa siku 30 tu

Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amefunguka kuwa kutokana na usajili mkubwa ambao klabu hiyo imeufanya wakiwemo washambuliaji Wakongomani, Heritier Makambo na Fiston Mayele, kikosi chake kinahitaji angalau siku 30, ili kutengeneza muunganiko mzuri.

Mpaka sasa Yanga wamekamilisha usajili wa wachezaji wapya 11 kuelekea msimu wa 2021/22 ambao ni Dickson Ambundo, Yusuph Athumani, Erick Johora, David Bryson, Diarra Djigui, Yannick Bangala Litombo, Khalid Aucho, Djuma Shabani, Jesus Ducapel Moloko, Makambo na Mayele.

Katika usajili huo, Makambo na Mayele wanapewa nafasi kubwa ya kuanza kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga, nafasi inayotazamwa zaidi hasa kutokana na changamoto waliyonayo kwa misimu miwili iliyopita.

Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi amesema: “Hivi karibuni tulikuwa na kambi ya muda mfupi nchini Morocco, kambi ambayo kwa kiasi kikubwa imetusaidia kujenga utimamu wa miili ya wachezaji wetu, sina shaka sana na wachezaji ambao tumewasajili kwa kuwa ni wale ambao tumekuwa tukiwafuatilia kwa muda mrefu.

“Lakini lazima nikiri kuwa tunahitaji muda wa angalau siku 30, kutengeneza muunganiko wa kitimu kwa sababu kundi kubwa la wachezaji ni wapya na pia wamekuja kwenye nchi ambayo ina utamaduni mpya wa soka.”nadhani nikishakuwa huko nitawaeleza,” amesema Chambeshi ambaye anaifundisha pia timu ya vijana ya Zambia.