Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 23Article 553018

Habari za michezo of Monday, 23 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mastaa nane wampasua kichwa kocha Nabi Yanga

Mastaa nane wampasua kichwa kocha Nabi Yanga Mastaa nane wampasua kichwa kocha Nabi Yanga

Kocha wa Yanga Nesreddine Nabi amesema kutakiwa kuondoka kwa wachezaji wake nane katika kambi yao kimemuumiza kichwa na kwamba anahofia muda mfupi wa maandalizi kabla hawajashuka uwanjani.

Nabi amesema licha ya kuopata muda wa kuwa na wachezaji wake hapa nchini Morocco lakini bado muda haukutosha kuweza kukamilisha kutengeneza alichotaka kufanya.

Kocha huyo raia wa Tunisia amesema hatua ya kundi la wachezaji wake kumeguka litazidi kuwaharibia kutokana watarejea zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kushuka uwanjani kucheza na Rivers United ya Nigeria.

"Tumekuwa na wakati mzuri kidogo hapa lakini hatujakamilisha ambacho tulitaka kufanya hapa na hii ya wachezaji kutakiwa kuondoka ndio inaniumiza kichwa zaidi tutapoteza muda zaidi.

"Tumemaliza ratiba ya kwanza katika kile ambacho tulitaika kufanya lakini kuna kazi tulitakiwa sasa tuwe pamoja katika kuikamilisha ili tuwe bora zaidi uwanjani na sasa unaambiwa kuna kundi linatakiwa lazima liondoke.

"Hii ni Afrika hawa wachezaji watasafiri kwenda mataifa mbalimbali na huko itategemea ratiba za ndege katika kurudi watarejea tena kuungana na sisi siku chache kabla ya mchezo utaona hapo wakati mgumu ambao tunao.

Related Yanga yasitisha kambi Morocco, warejea Dar kwa mafungu Koffi kutumbuiza siku ya Wananchi Bangala atema checheTshishimbi: Kwa Yanga hii mtakoma!Wachezaji wa Yanga ambao wameitwa timu za taifa ni wale watano wa Taifa Stars ambao ni kipa Ramadhan Kabwili, mabeki Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, viungo Feisal Salum na Zawadi Mauya.

Wengine ni pamoja na viungo Mukoko Tonombe (DR Congo), Khalid Aucho (Uganda) na kipa Diarra Djigui (Mali) ambao wote wataondoka haraka kuwahi kambi ya mataifa yao.