Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 07Article 541363

xxxxxxxxxxx of Monday, 7 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Matola: Simba Kazi Bado Haijamalizika

Matola: Simba Kazi Bado Haijamalizika June 6, 2021 by Global PublishersKOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema licha ya ushindi dhidi ya Ruvu Shooting hawajabweteka kuwa wamemaliza kazi badala yake bado wana shughuli nzito ya kuhakikisha wanatetea ubingwa wao.

Matola alitoa kauli hiyo juzi Alhamisi mara baada ya kumalizika mchezo wao wa ugenini dhidi ya Ruvu Shooting na kufanikiwa kushinda mabao 3-0 katika Uwanja wa CCM Kirumba.Matola alieleza kuwa ilikuwa ni lazima waifunge Ruvu kutokana na wao kufungwa tena nyumbani na kupelekea maneno kuwa mengi sana.

“Tulichokifanya leo (juzi) hapa Kirumba ilikuwa ni kulipa kisasi na nashukuru wachezaji wangu wameweza kufanya hilo kwa usahihi kabisa na sasa ni kujiandaa na mapambano mengine ambayo yapo mbele na kuhakikisha tunatetea ubingwa,” alisema Matola.

Aidha kocha huyo aliwataka Wanasimba wote wakati huu wanapokaribia kutwaa ubingwa wa nne mfululizo kuendelea kuwa wamoja na mshikamano kwa kuisapoti timu yao ikiwa nyumbani kama njia ya kuongeza hamasa na kuhakikisha wanafikia ndoto zao.

STORI: OSCAR MIHAYO | CHAMPIONI

Join our Newsletter