Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 17Article 543247

Habari za michezo of Thursday, 17 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Mayay aeleza kilichofanya jina lake kukatwa urais TFF

Mayay aeleza kilichofanya jina lake kukatwa urais TFF Mayay aeleza kilichofanya jina lake kukatwa urais TFF

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mayay ameeleza kuwa aliwasilisha vitu vyote vinavyotakiwa ikiwamo vyeti lakini upande wa wadhamini hawakukamilika.

“Kati ya vitu vilivyotakiwa kuwasilishwa kama vile kitambulisho cha uraia, vyeti vya shule na barua za wadhamini watano, lakini mimi nimepata mdhamini mmoja,” Mayay.

Amesema kuwa amejitahidi kuomba udhamini katika klabu zote 18 za Ligi Kuu Tanzania Bara lakini mmoja ndiye alimuunga mkono.

“Nitaendelea kutoa mchango katika soka kwa nafasi nilikuwa nayo, pia nipo tayari kutoa ushauri kwa wagombea wakihitaji sera zangu nilizotakiwa kuwasilisha kipindi cha kampeni,” Mayay