Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 20Article 552595

Soccer News of Friday, 20 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mayele anawatamani Simba

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Fiston Mayele Mshambuliaji mpya wa Yanga, Fiston Mayele

Siku mbili baada ya kuanza mazoezi akiwa na kikosi cha Yanga kambini nchini Morocco, mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Fiston Mayele, amesema huwa anapenda kufunga mabao katika michezo muhimu na migumu, huku akiwatamani kinoma Simba.

Mayele ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Yanga kuelekea msimu ujao wa 2021/22 ambapo mshambuliaji huyo ametokea AS Vita ya DR Congo.

Juzi Jumanne, Yanga ilianza mazoezi yake nchini Morocco huku mastaa wengi wa kikosi hicho wakionekana kuwa na furaha akiwemo Fiston.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mayele amesema: “Mara nyingi napenda kufunga mabao katika michezo muhimu kwa timu yangu husika, wakati nikiwa AS Vita nilikuwa nikipenda kufunga bao katika michezo yote ambayo timu yangu ilikuwa ikicheza na TP Mazembe.

“Nilikuwa napenda nifanye hivyo kwa kuwa ilikuwa inaleta kumbukumbu isiyofutika kutoka na upinzani wa hizo timu.

“Kwa sasa nipo Yanga, mpinzani mkubwa wetu ni Simba, hivyo natamani pia nifanikiwe katika hili, naamini itakuwa ni furaha kubwa kwa Wanayanga kutokana na upinzani mkali wa timu hizo.

”Septemba 25, mwaka huu, Simba itacheza dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ambapo Mayele anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoingia uwanjani kusaka ushindi.