Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 24Article 553285

Soccer News of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mbeya Kwanza mtawaelewa tu

Salum Abdallah Chuku akisaini Mkataba wa Kuitumikia Mbeya Kwanza Salum Abdallah Chuku akisaini Mkataba wa Kuitumikia Mbeya Kwanza

Timu nyingi ngeni zinazopanda ligi kuu Tanzania Bara huwa haziwezi kudumu kwa misimu mingi wanarudi ligi daraja la kwanza ama Championship kama inavyoitwa, lakini safari hii huenda hali ikawa tofauti kwa Mbeya Kwanza.

Klabu ya Mbeya kwanza FC imefanikiwa kumsajili Salum Abdallah Chuku kutoka Nkana Red Devil FC ya nchini Zambia kwa mkataba wa mwaka mmoja, ikiwa ni katika kukiimarisha kikosi chao kuelekea msimu wa ligi kuu Tanzania Bara.

Wakati hayo yakijiri kumbuka siku chache zilizopita walimtangaza Habib Kiyombo kama mmoja wa wachezaji watakaokitumikia kikosi hicho msimu ujao , Kiyombo alikua akiichezea klabu ya mamelodi Sundowns ya nchini Afrika ya Kusini.

Rolland Msonjo mlinzi wa kati ambaye ni mchezaji Wa Timu Ya Taifa Ya Vijana (U23) tayari alishasaini kujiunga na Mbeya Kwanza Kwa mkataba wa miaka miwili pamoja na  Mizah Cristom Abdallah akitokea klabu ya Namungo FC.