Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573244

Habari za michezo of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mechi ya Simba na DTB yahairishwa

Mechi ya Simba na DTB yahairishwa Mechi ya Simba na DTB yahairishwa

MCHEZO wa kirafiki kati ya Simba na DTB FC uliopangwa kuchezwa leo saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Mo Simba Arena umeahirishwa.

Katibu Mkuu wa DTB Muhibu Kanu alisema Simba waliomba mchezo huo wa kirafiki ingawa kutokana na ratiba kubana wameamua kutocheza.

"Ni kweli wenzetu walituandikia barua ya kuhitaji kucheza na sisi lakini kocha mkuu Ramadhan Nswanzirimo akaona ni vyema wachezaji wapate muda wakupumzika maana walicheza Ijumaa," amesema Kanu.

Timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Championship inashika nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na alama 18, baada ya kucheza michezo nane.

Kwa upande wa Kocha wa Simba Pablo Franco anataka kuendelea kukiangalia kikosi chake kufuatia kukiongoza kwenye michezo miwili ikiwemo wa kirafiki dhidi ya kituo cha Cambiasso walipofungana mabao 2-2, na ushindi kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting wa mabao 3-1, katika uwanja wa CCM Kirumba.