Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 24Article 553480

Soccer News of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Metacha mnata uelekeo ni hapa

Aliekuwa golikipa wa Yanga, Metacha Mnata Aliekuwa golikipa wa Yanga, Metacha Mnata

Aliyekuwa golikipa wa Klabu ya Yanga, Metacha Mnata taarifa zinaeleza kwamba yu mbioni kujiunga na wakusanya ushuru wa Kinondoni timu ya KMC kwa msimu wa Ligi kuu Tanzania Bara 2021/2022.

Metacha kwa sasa ni mchezaji huru tangu alipoachana na Klabu ya Yanga mwanzoni mwa mwezi huu baada ya Mkataba wake wa Miaka miwili kumalizika.

Meneja wa Metacha, Jemedari Said amesema: “Mpaka sasa kuna ofa sita za timu ambazo zinahitaji huduma ya Metacha, timu tano ni za hapa nyumbani huku timu moja ikiwa ni ya nje ya nchi".

“Kuhusiana na KMC ni kweli ni miongoni mwa timu ambazo tupo kwenye mazungumzo nazo, siwezi kuweka wazi kuhusu wapi tumefikia katika mazungumzo hayo lakini muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi, nikuhakikishie kuwa Metacha hawezi kukosa timu ya kucheza msimu ujao.”Ulipotafutwa uongozi wa KMC kuzungumzia mipango yao ya usajili, Ofisa habari wao,

Mwagala amesema “Kwa sasa siwezi kuzungumzia taarifa za mitandaoni, lakini niwahakikishie kuwa hivi karibuni tutatoa taarifa rasmi ya usajili mzima.”

Metacha kwa sasa anasubiri kujiunga na kambi ya Timu ya Taifa inayojiandaa kwa michezo ya kufuzu kombe la Dunia mwezi ujao.