Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 09Article 584449

African Cup of Nations of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mfahamu muamuzi wa kwanza mwanamke kuchezesha AFCON

Salima Mukansanga, anakuwa mwamuzi wa kwanza mwanamke katika mashindano ya AFCON Salima Mukansanga, anakuwa mwamuzi wa kwanza mwanamke katika mashindano ya AFCON

Wanawake wakiwezeshwa wanaweza, Salima Mukansanga anakuwa mwamuzi wa kwanza mwanamke kusimama kati na kuchezesha mashindano ya AFCON.

Mwamuzi huyu kutoka Rwanda ataweka historia kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kama mwanamke wa kwanza kuwahi kuwa mwamuzi wa kati kwenye michuano hiyo mikubwa Barani Afrika.

Salima anakuwa miongoni mwa waamuzi wanne wa kike watakaosimamia mashindano hayo wakiwemo kutoka Cameroon Carine Atemzabong, Fatiha Jermoumi wa Morocco na Bouchra Karboubi ingawa wao hawatachezesha mechi.

Salima ni mzoefu na tayari amesimamia mechi kadhaa ikiwemo za Kombe la Dunia la Wanawake, Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake na Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF.