Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 26Article 539851

Habari za michezo of Wednesday, 26 May 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mgunda kuna Ligi ndani ya Ligi Kuu Bara

Mgunda kuna Ligi ndani ya Ligi Kuu Bara Mgunda kuna Ligi ndani ya Ligi Kuu Bara

KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amedai Ligi Kuu Bara imekuwa ngumu kutokana na ushindani wa kuwania kubaki na kutwaa ubingwa.

Coastal Union ipo kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja ikishika nafasi ya 16 kwa pointi 33 baada ya kucheza mechi 29, imeshinda nane, sare tisa na kupoteza 12, ikiwa imefunga mabao 19 na kufungwa 39.

Timu hiyo imebakiza michezo mitano, mitatu itacheza ugenini dhidi ya Simba, Tanzania Prisons na Mbeya huku miwili ya nyumbabi ni dhidi ya Kagera Sugar na Mwadui FC, ambayo tayari imeshuka daraja hadi Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Mgunda ameaiambia Mwanaspoti kwa njia ya simu kutoka Tanga kuwa ugumu wa ligi hiyo katika hatua hii ya mwisho unatokana na timu nyingi kupigana kubakia na nyingine zinataka ubingwa.

“Kuna ligi ndani ya ligi unaona kabisa kuna timu tatu zinawania ubingwa kuna nyingine zinataka kumaliza nafasi ya nne, kuna zile hazitaki kushuka daraja, ukiangalia ushindani hapo unaona kabisa lazima ufanye kazi ya ziada,” alisema Mgunda.

Alisema kwa sasa vijana wake wanaendelea kujifua kuhakikisha mechi zote zilizosalia wanaibuka na ushindi hili kubaki Ligi Kuu kwani hawataki kushuka daraja na mipango yao siyo kushuka ni kubaki na kuendelea kuweka heshima ya soka Tanga.

Alisema baada ya kuwa na mapumziko ya wiki tatu kabla ya kurejea dimbani Juni 18 mwaka huu ugenini kumenyana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya anaendelea kutumia muda huo kwa ajili ya kucheza mechi nyingi za kirafiki ili kuweka wachezaji wake fiti.

Mgunda aliwaomba wapenzi wa soka mkoani Tanga kuendelea kuwaamini na kutokata tamaa kwani timu yao ni nzuri itapambana na kubakia kwenye ligi.

Join our Newsletter