Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 01Article 560701

Soccer News of Friday, 1 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mipango ya Biashara inaanza na Ruvu Shooting

Biashara United, itamenyana na Ruvu Shooting, Biashara United, itamenyana na Ruvu Shooting,

Baada ya Kupoteza kwa Dodoma Jiji katikati ya wiki, Kikosi cha Ruvu Shooting leo majira ya saa 10 za jioni kitashuka dimbani kupepetana na Biashara United katika uwanja wa Karume Mjini Musoma.

Sasa Kocha wa Biashara United, Patrick Odhiambo amesema sare dhidi ya Simba nyumbani iliwavurugia mipango yao kama timu.

"Unajua mipango yetu msimu huu ilikuwa ni tushinde michezo yote ya nyumbani na kujikusanyia pointi 30 ambazo tungejumlisha na tutakachokipata ugenini ingetuweka kwenye nafasi nzuri ya ubingwa"

"Sasa Ruvu ndio ataanza kwa kutupa, pointi tatu atake asitake, ni mtu wa kwanza anaekwenda kuwajibishwa na mipango yetu" amesema kocha huyo

Bishara United ni miongoni mwa timu tatu zilizobaki katika mashindano ya Kimataifa kuiwakilisha Tanzania baada ya Yanga kutolewa.