Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 13Article 557194

Habari za michezo of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Miquissone Aahidi Makubwa Al Ahly, Aitaja Simba

Miquissone akitambulishwa Al Ahly. Miquissone akitambulishwa Al Ahly.

ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa Simba ambaye sasa amejiunga na mabingwa wa Afrika klabu ya Al Ahly ya Misri, Luis Miquissone amesema kuwa, ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye kikosi cha wababe hao wa Misri kutokana na uzoefu mkubwa alioupata akiwa nchini Afrika Kusini na ndani ya Simba.

Miquissone alikamilisha usajili wake na kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Al Ahly Agosti 26, mwaka huu akitokea kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba ambayo aliichezea kwa misimu miwili tangu msimu wa 2019/20 na 2020/21.

Wakati akiwa na kikosi cha Simba kwa misimu miwili iliyopita, Luis alifanikiwa kucheza michezo 37 ya Ligi Kuu Bara, na kuhusika katika mabao 25 akifunga mabao 12 na kuasisti mara 13.

Akizungumza katika mahojiano maalum Luis alisema: “Kwangu ni jambo kubwa kujiunga na klabu kubwa kama Al Ahly, hii ni ndoto ya kila mchezaji mwenye malengo ya kuwa mchezaji mkubwa, hivyo ilikuwa furaha kwangu kucheza dhidi ya Al Ahly nikiwa na klabu ya Simba kwenye Ligi ya mabingwa Afrika msimu uliopita.

“Nimejifunza mambo mengi nikiwa na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini lakini pia nikiwa na Simba kwa msimu miwili niliyokuwa Tanzania, naamini kuwa uzoefu nilioupata nikiwa Afrika Kusini na ndani ya Simba utanisaidia kufanya vizuri katika majukumu yangu nikiwa na Al Ahly.”