Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 18Article 552238

Soccer News of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Mjiandae kwa taarifa za kuikandamiza Simba" - Kamwaga

Kaimu Afisa Habari wa Simba SC, Ezekiel kamwaga Kaimu Afisa Habari wa Simba SC, Ezekiel kamwaga

Kaimu Afisa habari na Mahusiano wa wekundu wa Msimbazi, Simba SC, Ezekiel kamwaga amewataka Klabu , Wanachama na Mashabiki wajiandae kisaikolojia kwani kuna taarifa nyingi mbaya ,zenye kuleta taharuki na za kuzusha zitakazoelekezwa kwa mabingwa hao wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Kamwaga ameyasema hayo leo Agosti 18, alipokua akifanya mahojiano na kipindi cha Sports Arena kinachorushwa na Kituo cha Redio cha Wasafi Fm, na hasa alipoulizwa kuhusiana na taarifa zilizovuma siku chache zilizopita kuwa ameng'atuka katika nafasi yake .

"Nawaomba klabu, wanachama na mashabki mjiandae, kwa taarifa na hasa hasa za kuikandamiza simba, katika nyakati hizi za ubora na ukubwa wa Simba mtasikia mengi, sisi jukumu letu kama Klabu ni kutoa taarifa sahihi haraka iwezekanavyo kwa chochote kile kitakachokua kinazungumzwa".

"Kuna mtu juzi kaamka tu kaandika simba imefungwa goli tisa na waendesha boda boda bila hata kututafuta kujua kama ni kweli au la".amesema Kamwaga.