Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 586012

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mkude Apata Hasira

Mkude Mkude

KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude, amefunguka kuwa kuchaguliwa kwake kuwa Mchezaji Bora wa Simba kwa mwezi Desemba, kumempa motisha ya kuendelea kupambana na kuendelea kuwa mchezaji muhimu ndani ya timu hiyo.

Mkude alisema tuzo hiyo ni kama deni kwa mashabiki ambao wamemchagua hivyo anatakiwa kuendelea kufanya kazi zaidi ili asiwaangushe wale ambao waliona kuwa alifanya kazi kubwa kuliko wengine mwezi uliopita.

Mkude aliibuka Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Desemba (Emirate Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month), akiwabwaga wachezaji wenzake watano akiwemo Kibu Denis ambao walikuwa wameingia tano bora.

Mkude alisema: “Hii tuzo imenipa hasira na hamasa ya kuendelea kupambana zaidi ili kuonyesha kuwa nilistahili kuwa mchezaji bora kwa mwezi husika. Nitafanya kazi zaidi na ikibidi niweze kuchukua tena hii tuzo.