Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 12Article 551173

Soccer News of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mkwasa bado yupo yupo sana Ruvu

Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa

Klabu ya Ruvu Shooting yenye Makao yake Ruvu, Mkoani Pwani imesema ipo tayari kuanza msimu mpya wa ligi kuu bara kwa maandalizi waliyofanya mpaka wakati huu.

hayo yamesemwa na kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa "Masta" amesema atawatumia vijana waliopo ili waweze kumpatia kile anachokitaka, huku akisisitiza kabla ya dirisha kufungwa wataongeza baadhi ya vijana ili wakafanye kazi atakayowatuma.

Kuhusu kuendelea kukinoa Kikosi hicho, Mkwasa amesema mkataba wake upo safi kilichopo wanakamilisha baadhi tu ya vipengele vidogo vidogo lakini hana mpango wa kutimka katika kikosi hicho kwa msimu ujao.

wakati Mkwasa akizungumza hayo nyota wa kikosi cha Ruvu shooting, David Uromi siku ya jana ametambulishwa kama usajili mpya na timu ya Dodoma Jiji na alipotakiwa kulitolea maelezo Mkwasa alisema;

"Sina taarifa, lakini kama ni kweli ameondoka sio tatizo,nitaendelea kutumia vijana waliopo ila tu nimtakie kila la heri".