Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573232

Habari za michezo of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mo alitoa Sh bilioni 5.2/- msimu uliopita

Mo alitoa Sh bilioni 5.2/- msimu uliopita Mo alitoa Sh bilioni 5.2/- msimu uliopita

Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Utawala na Uendeshaji wa Simba, Yusuph Nassor amesema msimu uliopita mwekezaji Mohammed Dewji alichangia Sh bilioni 5.2 kwa ajili ya uendeshaji wa klabu

Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Simba leo Novemba 21, 2021 Yusuph Nassor amesema fedha hizo ni nje ya Sh bilioni 20 za uwekezaji.

“Kipekee naomba tumpatie cheti za shukrani. Hii ni nje ya ile Bilioni 20,” Yusuph Nassor.

Aidha, amesema kuwa msimu huu Mohammed Dewji amepanga kutoa Sh bilioni 5.1 na tayari ametoa Sh bilioni 1.5 na katika fedha hizo Sh bilioni 1.2 zimetumika katika usajili wa wachezaji.

“Mambo makubwa kwa CEO wetu ni hakubali kushindwa na jambo linalofanyika leo hakubali lifanyike kesho. Kiukweli anafanya kazi iliyotukuka" amesema Nassor.