Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573145

Habari za michezo of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mo atajwa bajeti ya Simba, apewa urais wa heshima

Mo atajwa bajeti ya Simba, apewa urais wa heshima Mo atajwa bajeti ya Simba, apewa urais wa heshima

Dar es Salaam. Mwekezaji wa Simba, Mohammed 'Mo' Dewji amerajwa kuhusika na bajeti ya klabu hiyo.

Yusuph Nassor mkuu wa fedha, utawala na utendaji wa Simba ameouomba uingozi impe cheti cha shukrani mwekezaji huyo aliyewahi kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kabla ya kujiuzulu.

Akisoma taarifa ya fedha, Yusuph amesema mwaka uliokwisha klabu iliingiza Sh12.1 bilioni na matumizi ilikuwa Sh12.3 bilioni.

"Mo alitoa Sh5.2 bilioni ambayo inakaribia nusu ya bajeti ambayo ni nje ya Sh 20 Bilioni za uwekezaji.

"Mwaka huu wa fedha klabu itaingiza Sh11.8 bilioni," amesema Yusuph bila kutaja matumizi ya mwaka huu wa fedha.

Amesema katika pesa hiyo, Mo Dewji ataingiza Sh5.1 bilioni na tayari amekwishatoa 1.5 bilioni na 1.2 bilioni ilitumika kwenye usajili.

Hata hivyo amebainisha kwamba klabu hiyo kama inahitaji kupambana kimataifa inapaswa kuongeza bajeti yake kwani haiwezi kushindana na klabu zenye bajeti ya Sh 80 Bilioni na zaidi.